Friday, April 13

Watoto kuua, then kufungwa kosa la nani?


Watoto wawili wa miaka 11 na 13 wamefungwa jela miaka sita (6) na Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, baada ya kukiri kumwua mtoto mwenzao mwenye umri wa miaka miwili. 

 Jaji aliamuru watoto hao wapelekwe katika shule maalumu ya watoto watukutu wanaotumikia adhabu ya kifungo jela iliyoko mkoani Mbeya. 

Watoto hao walitenda kosa hilo Julai 15 mwaka jana saa 10 jioni, jijini Mwanza., baada ya kukorofishana  na mwenzao ambaye ni kaka wa marehemu. Walimuua mtoto huyo kulipiza kisasi kwa kaka mtu kuiba gololi zao.
Walimuua mtoto huyo kwa kumfunga kamba mikononi na miguuni, wakamning’iniza kwenye mwembe na kumpiga kwaa matofali kisogoni na kusababisha kichwa kipasuke, hali iliyosababisha ubongo wake kutoka nje. .. stori nzima SOMA HAPA

Ila mi nauliza, hapa nani wa kulaumiwa wazazi, jamii nzima au? Ni muvi na mieleka tunayowaacha watoto wetu waangalie au?
Yaani malezi yametushinda hadi watoto wanauana au? Tunawafundisha watoto walipizane visasi kiasi cha kuuana? Tunaenda wapi?

No comments: