Friday, June 29

Likizo hii tulikua Mikumi!

Hata sijapiga hodi, ila kwa taarifa tu kwa wadau wa mji kasoro bahari ni kwamba wiki hii yooote toka  Jumapili tulikua mjini kwenu (tuko hadi Jumapili) na itabidi mtuzoee tu, maana daddy kahamia Moro, so this is our second home, n we r loving it...
So Jumanne tukajimuvuzisha Mikumi, utalii wa ndani. Xchyler alikua very exited kuona wanyama, hasa giraffe maana ndio his fav animal, Xyleen alikua wala hajui linaloendelea kashangaa tu amekurupushwa usiku wa manane. Ndio, ukitaka kuwafaidi wanyama aitha uende asubuhi sana au jioni sana, tulichagua asubuhi sana! So tumeingia tu kwenye gari, totoz wote usingizi!


kuona yaliyojiri huko mbugani bofya hapo kushoto...


Baba na mwana, na zebra!

Binti, uso kwa uso na elephant!

Sisi na kiboko!

Kaila anawaangalia hippo kwa makini, kama haamini vile...

Nilikipenda sana hiki kijiwe...kiko chini ya mbuyu unaokadiriwa kuwa na miaka 500!
Kasheshe ikawa kwa lion...kumpata kwanza ni bahati...sie tukawakuta wawili.


Kijana aliogopa mno, as yeye alidhani lion ni kama cat, loh, kumbe lion ni mkubwa hivyo na anakula nyama, nani anataka afanywe lunch?

Binti hakuwa na wacwac na lion...what does she kno?

Simba walikaa hapo muda mrefuuu, wote tukapata pozi nao, na tulikua karibu nao mno, as close as you can get to a lion in the wild!
All in all it was a wonderful experience, Tanzania tuna vitu vizuri sana, na sio expensive, kiingilio ni 1,000/-, hujaona vibaya wala sijakosea, ni buku tu kwa Mtanzania mtu mzima, watoto under five bure, miaka 5-10 ni 500/- tu! Kuingia na gari 10,000/- unaspend shingi ngapi kula bata kila wikend? Hii ni kidogo sana, unajitoa tu once unawaonyesha watoto what the real animals look like, sio mambo ya kudhani lion ni sawa na cat! Ingawa hakukosea sana - si wote cats!
Enjo your wikend!

2 comments:

Anonymous said...

Jiang! mmependeza sana.Mbona hujaweka jamani ile menu ya mtoto.pls naomba uweke

Anonymous said...

jiang pozi lako sijalielewa mana mguu umekua kama wa panzi, all in all superb family pic. X anakua handsome, Xpart 2 ndo mcute hadi raha. LOVELY PHOTO MGUU WAKO TU NDO NIMEUMIND