Monday, July 2

Unajua nini kuhusu chanjo za watoto?


Huwa tunabeba tu malaika wetu clinic tu kufuata ratiba iliyopo kwenye kadi zao. Kama siku hiyo ni kudungwa sindano haya, kama ni matone twende, na kuambiana mpe panadol kabla ya chanjo (zile za sindano) ili asipate homa, mara umwekee barafu…yes nimefanya yote hayo, ila sijui kama kuna ukweli kiasi gani kuhusu panadol na barafu. Pia sijui kama wote tunajua kazi ya hizo chanjo na zinafanyaje kazi.
Twende wote(bonyeza palipoandikwa ZAIDI BOFYA HAPA ») tuongeze maarifa…
Chanjo ni nini?
Chanjo ziliyotengenezwa ili kulinda mpewa chanjo (anaweza hata akawa mtu mzima kama chanjo ya manjano) dhidi ya ugonjwa fulani. Chanjo ni moja ya vitu muhimu sana katika makuzi ya watoto.

Chanjo zinafanyaje kazi?
Chanjo ni wale wale wadudu wanaoleta ugonjwa huo, wanaingizwa mwilini wakiwa labda wamepunguzwa makali au wameuliwa fulani hivi, so mfano chanjo ya polio, ni walewale wadudu wa polio wanaingizwa mwilini wakiwa wamepunguzwa makali.  
Wadudu hao wakishaingia mwilini, mwili wako unatengeneza antibodies dhidi ya ugonjwa unaosababishwa na wadudu hao.

Hizo antibodies zikishatengenezwa huwa zinabaki, kiasi kwamba huo ugonjwa ukiingia au ukilipuka hauwezi kumwathiri mtu ambaye tayari alishachanjwa, maana antibody zile zilozokwishatengenezwa kwa kutumia wadudu dhaifu zinawashughulikia hao wadudu wa ukweli.

So chanjo ni muhimu sana, maana zinamhakikishia mtu kinga ya magonjwa mbalimbali most of the time kwa maisha yake yote. Magonjwa hayo mara nyingi huwa ni makali, mengine hayana dawa, so ukiwa hujachanjwa ukikupata ni balaa. Pia magonjwa mengine yamepotea nchi fulanifulani, kama polio Tanzania inaelekea kupotea (I stand to be corrected), kwa sababu ya kuzingatia sana chanjo. Na mengine hatuyaoni sasa hivi kwa sababu karibu watu wote wanachanjwa wakiwa wadogo, so mlipuko utoke wapi, labda uje na mtu wa nchi nyingine.

There we have it kuhusu chanjo ni nini…unataka kujua ratiba ya chanjo za muhimu/lazima kwa watoto wote, ambazo huwa wanapata kuanzia wanapozaliwa hadi wanapotimiza mwaka mmoja…be here next week, siku kama ya leo. 

1 comment:

Anonymous said...

Jiang, wenzetu huku nje, yaani ukifika hayo machanjo wanayo ongezea watoto utawaonea huruma. Kumbe chanjo zote tunazofanya huko nyumbani, zinatakiwa ku booster kila baada ya miaka kadhaa, kasoro BCG.