Thursday, June 28

Mwanao ana adabu?


Watoto wanakua kadri tunavyowafundisha. Unaweza ukakutana na mtoto wa mtu ukafurahi, mtoto ana adabu hadi unahadithia. Adabu hainyweshwi kama dawa, so naamini hamna mtoto mwenye adabu aliyejikuta tu ana adabu, lazima amefundishwa. 
Ingawa haimaanishi mtoto asiye na adabu hajafundishwa, maana malaika wetu tunawapenda, ila wengine ni wabishi sana kufundishika, hasa vitu vizuri. Ni bora tukawafundisha, tangu mapema, sio unasubiri siku ya kitchen party ndio unaanza; ‘mwanangu, kuna maneno makuu matatu ya kuzingatia kwenye ndoa…" jamani, ina maana mdada wa miaka 25 alikua hayajui? Maana kama ameshazoea kutumia neno samahani kwa watu aliowakosea, basi atatumia hata kwa mumewe.

Umuhimu
Umuhimu wa adabu ni mwanao kupendwa, na wakubwa na watoto wenzie. Mtoto asiye na adabu hata wenzie hawatampenda, so ataumia socially, kwa kuona hapendwi tangu mdogo.
Pia, asipokua na adabu atakutia aibu! Unaishia tu; “jamani, fulani mbishi sana” wakati kagoma kuamkia, tena kwa ukali ‘Sitaki!’
Mtu mwenye adabu huwa anapendwa na watu wote; so hizi ni must-do-manners, ambazo mwanao muhimu awe nazo…

(Bofya hapo kushoto uzione...)


Shikamoo
Kibongobongo, kwa Kiswahili chetu na lugha za makabila mbalimbali, ni wajibu wa mdogo kumwamkia mkubwa… mtoto ajifunze kuamkia wakubwa mapema asije akakutia aibu!

Naomba
Akihitaji kitu atangulize neno naomba; hata kwa dada. Sio “dada nipe maji”, NO, ni “dada naomba maji”

Asante 
Akipokea kitu aseme asante. Akifurahia kitu alichofanyiwa na mwingine aseme asante.

Samahani
Mfundishe mtoto kusema samahani akikosea, sio labda unamchapa au kumgombeza then kila mtu anachukua time zake. Muhimu kuomba msamaha kwa mtu aliyemkosea. Pia hata kwenye situation zingine, kama kumkanyaga mwenzie kwa bahati mbaya.
Ila make sure, akishajua thamani yake, samahani anaimaanisha. Mi naombwaga msamaha na kuambiwa ‘mama sichezi na wewe’ at the same time…hapo anakua haoni kama amefanya kosa na anaomba samahani coz nimemwambia! Sasa ndio inabidi mjadili what is wrong… ni muhimu kumfundisha mtoto kujiexpress, coz ukimfundisha awe ananyamaza hata kama anaona ameonewa, ndio ata grow up na low self confidence, na u know the world is never fair!

Pole
Ni tabia njema kuwaambia mtu pole anapopata jambo ambalo si zuri; kama kuumia. So mtoto natakiwa kulijua hili neno mapema.

Hodi
Do I need to say athari ya hii? Ni mambo ya kukutwa mnatengeneza mdogo wake… mfundishe awe anapiga hodi kwenye kila mlango na kusubiri, ili kila mtu awe na privacy…ila pia na wewe mzazi uwe unapiga hodi chumbani kwake/kwao, maana manners huwa hazina umri!

Matusi
Utake usitake mtoto atasikia na atayajua matusi! Iwe kwenu nyie wazazi sometimes bila wenyewe kuwa aware kwamba anasikia na anaelewa, au kwa wenzake shule au mtaani tu…uswahilini kwetu tena mama fulani anapandishiana na mama fulani, matusi ya nguoni nje nje, watoto wataacha kuyashika?
Ukitaka kujua anayajua subiri siku atukanwe, atakuambia fulani kanitukana, amejuaje kama ni tusi? So kujua matusi si issue, as huwezi kuzuia kama tunaishi kwenye jamii!
Naamini kila mtu anayajua matusi; tunatofautiana ujuzi wa kuyapanga tu! Wanaoonekana hawana adabu ni wale wanaoyatumia ovyo, tena hadharani! Sasa hapo, mfundishe mwanao kwamba matusi si maneno ya kutamkwa ovyoovyo, wala si maneno mazuri! Katika hili mi ni mkali sana, maana anaweza akakutukania wageni kisa wamebadili channel ya katuni, sijui utajificha wapi!
Hii ni pamoja na kutumia mean names; jamani mtoto mdogo anaita mwenzie mbwa we! Kama unamwitaga mbwa ukikasirika na yeye atalitumia tu akikasirika!

Kuheshimu ma-dada aka mayaya:
Jamani, just because unamlipa mshahara sio ndio mwanao awe anamtreat like nothing! Huko ni kukosa adabu! Amuheshimu dada kama anavyokuheshimu wewe, akiwa na tatizo naye au akiona hamtendei haki, amsemee kwako na wewe utalishughulikia.
Kwenye mahusiano wanasema ‘To know how he will treat you in the long run, look at the way he treats people who do not mean much to him, like waiters’, this also applies to watoto wetu, akiwa hana adabu kwa hao wanamlisha na kumvisha kuna siku atakukosea adabu na wewe tu!

Kutoingilia watu wakiongea: 
Hasa wakubwa, mtoto ajifunze debating skills, asiongee mtu mwingine akiwa anaongea, asubiri akimaliza naye ndio aongee, watoto wanapenda sana hii wakiwa wanashtakiana. Of course ikiwa emergency ni kitu tofauti.

Kuomba ruhusa:
Mfundishe mtoto kuomba ruhusa anapotaka kufanya mambo yake kama kwenda kucheza nk. Mkubalie kinachofaa, unachoona hakifai toa sababu za msingi… believe me, utapunguza kuruka ukuta kwenda disco akikua maana anajua kabisa wazazi hawapendi mambo fulani na kwa sababu hizi!

Kutosema vibaya ulemavu wa watu:
Watoto hawalifanyi hili kwa nia mbaya, ni kwa sababu hawajui ndio utaona sometimes wanatoa maoni kuhusu ulemavu wa mtu, tena kwa sauti…sasa inatiaga aibu sana kwa mzazi mwanao akifanya hivyo…so mfundishe kuwa ulemavu ni maumbile tu wenye ulemavu hawajapenda kuwa hivyo na si vizuri kusemasema kuhusu hilo hata kama ni kwa kumwonea mtu huruma.

Kufunga mdomo anapopiga chafya au anapokohoa:
Hii ni tabia njema, pia kiafya ni nzuri…maana ndio mambo ya vikohozi kutoisha ndani kwenu, mkubwa anamwambukiza mdogo, then mdogo to mkubwa!

Balance!
All this said naomba tukumbuke kwamba binadamu, watoto included, ana FREE WILL! Yes, hata Mungu katoa vitabu tujifunze weee, ila tuna utashi wa kufanya tunachotaka. Unavyomfundisha mwanao adabu kumbuka pia kumjengea confidence na kujiamini. Asije akawa na adabu hadi anakubali kubakwa coz ushamfundisha akubali kila kitu anachoambiwa na mkubwa!
Thus why ni muhimu kubalance haya mafunzo, na mjengee mtoto uwezo wa kusema no…will talk about haki za mtoto next time. 

For now, share nami, incidents ambazo mwanao alizokuacha ukitamani ardhi ipasuke kwa kukosa adabu au ambazo mtoto wa mtu alifanya, si tunakutaga kwenye sherehe na clinic tunaona!
Kuna niliyosahau? Niliyopitiliza je? Tiririka kwenye comments!

2 comments:

frank manata said...

Hii safi sana hongera dada.

Anonymous said...

hongera sana mama x.umenikuna sana na haya mafundisho nitayazingatia.wa mama jamani tuwe makini na watoto wetu