Unashangaa? Yes, unaweza kumfanya mwanao awe smart kwa
chakula tu! Ndio coz kuna vyakula vinarutubisha ubongo kuliko vingine, sasa ukivikazania hivyo utakuta mwanao anakua
smart kuliko wengine wasiokula vyakula hivyo. Huamini? Basi bonyeza hapo
palipoandikwa bofya hapa utiririke namie.
Siri iko kwenye kifungua kinywa!
Kibongobongo tunaita chai, ila kwa Kiswahili sanifu ni
kifungua kinywa. Hiki wataalam wanasema kazi yake si kufungua kinywa tu, hata
ubongo unafunguka. Tafiti zinaonyesha kuwa watoto wanaopata kifungua kinywa
wanafanya vizuri kwenye test za kuangalia attention na kumbukumbu, kuliko wale
wasiopata kifungua kinywa. Na wote tunajua, attention darasani ndio inamfanya mtoto
aelewe, afu kumbukumbu ndio inamfanya afanye vizuri kwenye mtihani au hata
application ya vitu alivyojifunza baadae. So bila hivyo vitu viwili mtoto kufanya
vizuri darasani si rahisi.
Kwa nini chai/kifungua kinywa?
Kwa sababu chakula ndio mafuta ya miili yetu, sasa mtoto anamka
mafuta yamepungua, inabidi ajaze tank lake (tumbo) ili kila kitu kiende sawa,
including brain yake.
Ila sio kila chakula kina the same effect. Lakini kitu
chochote ni better than nothing, maana watoto wengine wanachagua sana vyakula.
Baadhi ya vyakula vya kurutubisha ubongo:
- Peanut butter (siku hizi ziko kibao, mini market yeyote unapata)
- Mayai
- Ndizi mbivu
- Maziwa
- Mtindi
- Asali (unaweza kuipaka kwenye mkate)
Hadi hapo tuko sawa ….kupata tips nyingine ya kuongeza
akili za mwanao ungana name same day next week. Kama ulipitwa na iliyopita,
click kwenye tab ya Elimu hapo juu.
No comments:
Post a Comment