Tuesday, June 26

Matokeo ya poll ya umri wa kumuanzisha mtoto darasa la kwanza

Wiki yote iliyopita ulipigia kura swali; 

WATOTO WAANZE DARASA LA KWANZA LA PRIMARY SCHOOL WAKIWA NA MIAKA MINGAPI?


Ulipiga kura yako? Kama hukupiga pole, ila nyingine inakuja soon, so shiriki kuchangia maoni yako kwenye inayokuja. Ukute hata hujaona matokeo, well matokeo ni haya:
Wadau wengi, asilimia 50 ya wote waliopiga kura waliona mtoto aanze shule ya msingi akiwa na umri wa miaka mitano (5), wakati asilimia 40 waliona umri wa kuanza shule ya msingi unaofaa ni miaka sita (6) na asilimia kumi tu ndio waliona umri huo uwe miaka saba (7).
Mimi binafsi niko kwenye kundi la miaka sita...naona kama miaka 7 anakua amechelewa kidogo, na miaka 5 kama amewahi kidogo...najua kila mtu una maoni yako kuhusu upande unaopendelea, tiririka...

Afu usisahau kupigia kura poll mpya eeh...nairusha muda si mrefu.

No comments: