Monday, June 25

Massawe wengine hawa hapa!

Niliuliza hapa karibu wiki mbili zilizopita, kama kuna Dr Massawe mmoja tu mji huu...nimepata majibu mazuri sana, sasa kwa faida ya waliokosa yaliyopita, huku nikiongezea ya rafiki zangu wa Facebook, hii ndio list ya Massawe aka pediatricians aka madaktari bingwa wa watoto wanaopatikana Dar es Salaaam...sorry, wadau wa miji mingine, sikupata hata comment moja kuhusu hilo, so kama kuna mtu anawajua wengine wa miji mingine, tusaidiane tu kuhabarishana...Jina la doctor
Anakopatikana
Comment kuhusu upatikanaji
Dr Massawe
Anapatikana Muhimbili.

Pia ana clinic binafsi pale Morocco, anakopatikana kuanzia jioni.
Jitayarishe kuwahi foleni usiku wa manane.

Dr Dulla, Dr Anthony na Dr PamphilHawa wote wanapatikana Morocco kwenye clinic ya Dr Massawe
Hawa hawana foleni.
Dr Namala
Anapatikana Muhimbili.

Pia ana clinic binafsi Upanga.
Huyu kumuona ni kwa appointment so no foleni kabisa, jitayarishe tu vizuri na pochi nene.
Prof Kareem
Pia ana clinic binafsi Upanga.
Kuna foleni.
Dr Hameer
Ana clinic yake Kariakoo
Kuna foleni si kidogo, ukifika saa tatu, imekula kwako.
Dk Swai

Muhimbili

Dk Emanuel
Regency

Dk Kuboja

Muhimbili.

Pia anapatikana Aga Khan.

Dr Ruta
MOI

Prof Kahamba
MOI

Dk Kisenge

AAR ya Morocco 

Pia anafundisha MUHAS

Dr. Kaja
M/Nyamala Komakoma

Dr. Hasanali
Mtendeni Clinic, Karibu na Mtendeni Primary school maeneo Kisutu.

Pia anapatikana Trauma Centre, Masaki.
Hakuna foleni za kutisha
Dr. Yohana
Clinic yake iko pale Elia Complex opposite na chuo cha CBE
Hana foleni za kutishaNimeondoa comment zote kuhusu ubora wa hawa madaktari. Kwa ujumla wote hawa wanasifika kwa kutibu watoto vizuri, na ni kutoka kwenye personal experiences za wadau. 
Disclaimer: 
  • Naomba ieleweke kwamba hizi ni comment za wasomaji, sijui ubora wa hao madaktari, as sijawahi kupeleke wanangu zaidi ya Massawe. 
  • Sijalipwa na wala simjui wala hanijui daktari yeyote niliyemlist hapo (hata huyo Massawe am sure kanisahau--he only saw me once), this is purely audience generated. 
  • Hii haimaanishi kwamba hakuna madaktari wengine wazuri kama hawa au hata zaidi ya hawa, ila hawa ndio niliowapata kwenye comment za watu, kama una unayemjua tafadhali tujuzane. 
  • Nia ya hii post sio kutangaza madaktari bora zaidi, nia ni kutanua wigo wa kupata huduma hii ya muhimu, ambapo most of the time it is the matter of life n death ya malaika wetu, roho zetu, our everything, so yes it matters that we go to VERY GOOD doctors! 
  • Kama una experience mbaya ambayo unadhani ilisababishwa na uzembe wa mmoja wa huyu daktari niliyemlist hapa, naomba nitumie email tulijadili. Ila tusitaniane, hiki ni kitu cha kuwa makini sana.

1 comment:

Anonymous said...

hello dear also kuna dr.msomekela alikua muhimbili kastaafu anapatikana sinza palestina hospital yake inaitwa amen ni mzuri sana