Friday, June 15

Simba wararua mtoto Bahari Zoo, Dar


Newton akiwa na mama yake, Veronia (kwa hisani ya familia ya Newton)



Hii stori imenitishaje? Maana ukizingatia nimetoka zoo na watoto kibao juzi tu. Ama kweli umakini ni muhimu sana tunapokua na malaika wetu...
Nimeiweka kama nilivyoitoa kwa waandishi wa Jumuia ya Waandishi wa Habari Tanzania (Tajoa). Read on...

MTOTO Newton Titus (5) wa Gongolamboto, Dar es Salaam amejeruhiwa vibaya na simba anayefugwa katika shamba la wanyama la Bahari Zoo, lililoko Tegeta, katika jiji hilo.

Tukio hilo limetokea Ijumaa iliyopita wakati mtoto huyo anayesoma chekechea, akiwa ameongozana na dada yake, walipoenda Bahari Zoo kutazama wanyama pori wanaofugwa katika shamba hilo.

Akizungumza jana na Jumuia ya Waandishi wa Habari Tanzania (Tajoa) yenye makao yake makuu Njombe, baba wa mtoto huyo, Titus Mchunga alisema kuwa mtoto wake alitamani kwenda kutazama wanyama, hivyo aliruhusu aongozane na dada yake kwenda Bahari Zoo ili kutimiza azma yake.

Titus, akielezea tukio lilivyo, akimnukuu dada aliyeongozana na mtoto wake kwenye shamba hilo la wanyama, alisema Newton alishambuliwa na simba huyo aliyekuwa ndani ya tundu lake, baada ya kujisogeza karibu naye.

(kujua ilitokeaje hadi akararuriwa na simba bofya hapo kushoto palipoandikwa ZAIDI BOFYA HAPA)

Baba wa mtoto huyo aliendelea kueleza zaidi kwamba anachokiona katika shamba hilo ni uzembe wa watendaji wake, hata kusababisha mtoto wake kukumbwa na shambulio hilo baya lililohatarisha uhai wa mtoto wake.

“Baada ya ajali hiyo, Newton alipiga sana kelele na kugaragara akiwa anatokwa damu kila sehemu ya mwili wake kuanzia kichwani hadi kwenye miguu, ndipo dada yake alimkimbilia na kumuokoa akiwa anasaidiana na mgeni mwigngine katika shamba hilo, dada wa Kihindi, ambapo walimchukua na kumpeleka hospitali ya jirani alikopata matibabu, hasa kwa kushonwa nyuzi kila sehemu,” aliongeza baba huyo kwa uchungu.

Alisema mtoto wake baada ya tiba aliruhusiwa na kurejea nyumbani na hata sasa hali yake ni mbaya.

Baba huyo kwa kuona hali ya mtoto ni mbaya, ameamua kuchukua hati ya ruhusa ya matibabu kutoka Kituo cha Polisi cha Wazo, ili aendelee na matibabu zaidi.

Bahari Zoo wanasemaje?

Mmiliki wa shamba hilo la wanyama, Wilson Kusaga akizungumza na Tajoa amekiri mtoto huyo kuparuriwa na simba, huku akimlaumu dada aliyekuwa amengozana naye kutembelea wanyama hao.

Kusaga amesema tukio lilitokea Jumamosi wakati yeye na familia yake wakiwa kanisani na kuwaacha waangalizi wa wanyama hao kwa ajili ya kuwapokea wageni na kuwatembeza shambani kujionea wanyama.

Amesema, kilichotokea, baada ya kusimuliwa na mwangalizi aliyekuwepo wakati wa tukio ni kwamba, dada aliyekuwa na mtoto huyo alimuacha akiwa peke yake mbali kidogo na matundu ya wanyama naye akaenda kujisaidia.

“Mtoto akiwa ameachwa peke yake, alijisogeza kwenye tundu la simba wawili ambapo ukaribu wake ulitoa mwanya kwa simba hao kumshambulia kwa kutoa mikono yao na kuanza kumvuta karibu zaidi.

Amesema dada aliyeongozana na mtoto huyo, ambaye alikuwa mwangalizi wa wanyama hao kipindi cha nyuma, hakuwakabidhi mtoto huyo waangalizi na alikuwa akimtembeza mwenyewe Newton kuwatazama wanyama.

“Huyu dada alikuwa anawatunza hawa simba na wanyama wengine, aliacha kazi, sasa nadhani akaona kuwa ahitaji msaidizi, na hata alipoenda kujisaidia alimwacha tu bila kumkabidhi na kwa kuwa watoto ni wadadisi, aliamua kusogea kwenye simba na ndipo walipomshambulia, nasikitika sana kwa tukio hilo,” aliongeza Kusaga.

“Zaidi sana kilichotokea ni uzembe tu, mbona tumekuwa tukipokea watoto zaidi ya 20, 000 tangu tuanze kazi hii na hakuna tukio lolote baya lililotokea na bado watoto wengine wadogo zaidi wanakuja na kufurahia wanyama, huyo mtoto alivuka wigo unaozuia watu kukaribia wanyama wakali, inasikitisha sana lakini,” amesema Kusaga.

Kusaga amesema kuwa mtoto alihudumiwa kwa gharama zake na kwamba wako radhi kuendelea kumhudumia hadi atakapokuwa amepona.

Mmiliki huyo alimuomba baba wa Newton kutoa ushirikiano naye ili mtoto aweze kuhudumiwa zaidi ili apone na aache tabia ya kulalamika kwani anayo nafasi ya kuzungumza naye ili kuona namna wanavyoweza kumsadia zaidi mtoto apone.

Wakati marafiki wa Tajoa mkiendelea kutafakari Bajeti, ni vyema pia tukazungumza kuhusu tukio hili la kusikitisha. Tafadhali changia mawazo yako nini kifanyike kuzuia matukio ya namna hii kutokea na ushauri gani mnatoa kwa mmiliki wa shamba la wanyama na baba wa mtoto aliyejeruhiwa.

Chanzo: Waandishi wa Tajoa. 

3 comments:

Joy said...

Nimesikitika kwakweli ila ninalaumu system nzima ya hiyo zoo. Kule kigamboni kila sehemu yenye wanyama wakali kuna mtu anayetoa maelezo na nadhani hata wao wanaitaji kufanya ivi.

Wakisema wao walienda kanisani na wakaacha msaidizi manake waliacha mz=saidizi mmoja for the whole Zoo? Havent been to the ZOO but nadhani its wise kuweka waangalizi wa wanyama to every area ambayo ina wanyama wakali.

Anonymous said...

Wazazi tume makini sana hasa tunapoamua kuwatoa watoto wetu aouting ni vizuri na wenyewe tukawepo ili kukwepa madhara kama haya na siyo kuwaachia watu wadada majukumu ya kila kitu kwa watoto wetu.Nimesikitika sana pia ni wajina wa mtoto wangu Get Well Soon Newton

Anonymous said...

kwa kweli mimi nawalaumu sana hawa wenye zoo; inaonyesha kabisa zoo yao haipo makini; natoa wito kwa mamlaka husika kuwawajibisha kwa jambo lilotokea.