Thursday, July 5

Mdau ni ma-shoto au ma-lia?

Unajua kuwa si rahisi kufahamu mkono atakaotumia mwanao hadi akifikisha miaka miwili, sometimes hata mitatu. Yes, usiseme mashoto yet, subiri kidoooogo! Akifika miaka miwili ndio utaona waziwazi mkono anaopenda kuutumia zaidi. Na wengine, hasa wale left handed wanaweza wakawa wanatumia yote miwili, mfano kula mkono wa kulia, lakini kuandika kushoto, hadi miaka 6 hivi ndio anakua mashoto kamili!



Nini kinamfanya mtoto awe ma-shoto au ma-lia?

Geneticis! Kama wazazi wote wawili mnatumia mkono wa kushoto, basi uwezekano wa mtoto wenu kuwa mashoto pia ni asilimia 45 hadi 50! By the way, watu wachache sana ya watu ndio left handed, ni asilimia 10 tu ya watu wote!



Kama you cant wait kujua mkono atakaokuja kutumia mwanao, mpe kitu, au msogezee kitu, kiwe katikati, atakichukua na mkono atakao tumia, jaribu mara nyingi utajua.



Wataalam wanasema kama mtoto anaelekea kupendelea sana kutumia mkono mmoja, bila kutumia mwingine, kabla hajatimiza miezi 18, ongea na mtaalam wa watoto, inaweza ikawa dalili za matatizo kwenye mkono huo mwingine.



Afu usilazimishe mtoto kutumia mkono asiopenda kutumia. Kwanza hamna tatizo lolote mtu akiwa left handed (kiukweli mi naonaga ni bonus hasa kwenye michezo!). Pili sio tu genetics zinazochangia mtoto kutumia mkono huo, ni pamoja na wiring ndani ya ubongo wake (huwa wanasema, left handed people huwa wanatumia upande wa kulia wa ubongo kuliko right handed). So kumlazimisha atumie kinyume na ubongo wake ulivyosukwa kunaweza kumchanganya na kum-frustrate tu, afu pia inaweza kumchelewesha kujifunza, hasa kuandika, inayoweza kumfanya ajione hana akili, kumbe anazo!


2 comments:

Anonymous said...

Aahhahaa duh...mimi ni mashoto ngoja nikamtest mtoto wangu nione atatumia mkono gani...but anapenda sana kula kwa mkono wa kushoto and she is turning 2yrs next month!!!!

Nimeamini ni genetics mana kwetu tupo mashoto wa3 na mama yetu na anko zetu wengi ni mashoto

jfk said...

Binti yangu ana miaka 18 sasa ni mashoto, ilikuwa nina ugomvi na mwalimu wake wa nasari ambaye alikuwa anataka kulazimisha awe Ma-lia. Nikamuweka kikao aache kabisa kulazimisha watoto kubadili mkono anawaharibia maisha , nilishukuru baadae sana alipokuja kukiri kuwa alidhani anasaidia kumbe kagundua alikuwa anaharibu