Monday, July 9

Ratiba ya chanjo


Last week niliongelea umuhimu wa chanjo, sina haja ya kurudia leo (kama hujui bofya kibufe cha AFYA hapo juu utaona) ila swali ni; mama na baba mtarajiwa hivi mnajua mlolongo wa chanjo atakazo zipitia mwanenu kabla ya kufikishwa mwaka mmoja. Yaani atadungwa sindano kabla ya kujua kusema tata… unajua lini anatakiwa apate chanjo hizo? Unajua hizo chanjo zinazuia nini?

Bofya palipoandikwa ZAIDI BOFYA HAPA » upate ratiba nzima ya chanjo za muhimu na zinachozuia.
Ratiba ya chanjo kwa watoto wa umri chini ya mwaka mmoja:

Umri
Aina ya Chanjo
Ugonjwa Unaozuia
Sehemu Inapotolewa
Kuzaliwa
Kifua kikuu (BCG)

Polio
Kifua kikuu

Kupooza
Bega la kulia

Mdomoni
Wiki ya 6
Polio 1

Pentavalent
Kupooza

Dondakoo, pepopunda, kifaduro, homa ya ini, homa ya uti wa mgongo na kichomi
Mdomoni

Paja la kushoto
Wiki ya 10
Polio 2

Pentavalent
Kupooza

Dondakoo, pepopunda, kifaduro, homa ya ini, homa ya uti wa mgongo na kichomi
Mdomoni

Paja la kushoto

Wiki ya 14
Polio 3

Pentavalent 3 (Dtp – hep b – hib)
Kupooza

Dondakoo, pepopunda, kifaduro, homa ya ini, homa ya uti wa mgongo na kichomi
Mdomoni

Paja la kushoto

Akikamilisha miezi 9
Surua
Surua
Paja la kuliaHii nimeitoa hospitali flani hivi, ilikua imebandikwa kama tangazo kutoka wizara ya afya. According to the tangazo, chanjo hizi zote ni salama na ni bure kwenye hospitali zote, private na public. Ingawa nimekopi kadri ya uwezo wangu mnisamehe kama nimekosea spelling za medical terms, maana mie sio dokta, but I hope nimesaidia wazazi wenzangu kupata general knowledge kuhusu hizo chanjo.

3 comments:

Mfalme Mrope said...

ahsante sana dada kwa habari. wazazi na tuzingatie chanjo hizi kwani muhimu saana kwa afya za watoto wetu...

Anonymous said...

hongerav mama x .umetusaidia wa mama .mi ni mama na mwanangu kapata chanjo zote.lakini nilikua sizijui maana yake.asante kw kutujuza

Anonymous said...

hongerav mama x .umetusaidia wa mama .mi ni mama na mwanangu kapata chanjo zote.lakini nilikua sizijui maana yake.asante kw kutujuza