Thursday, August 23

Kidole...kizuri au kibaya?

Kaka na dada...yes, na binti naye siku hizi ananyonya kidole, tena yeye ni kushoto na kulia, ukimtoa hiki, anaweka hiki!
Hili lishaonekana kama nalo ni janga la kitaifa...hivi ni janga au baraka?
X mkubwa alianza tangu alipozaliwa, Xy yeye ameanza juzi juzi tu, hata ilipotokea sijui...
Nilikua nalalamika sana kuhusu X kunyonya kidole, hadi leo sikipendi, ila kiukweli kwa Xy naona kimemfanya aache usumbufu wakati wa kulala. Tangu aanze kunyonya kidole ukimuweka kitandani tu ananyony kidole chake huku analala mwenyewe.
Swali ni je, kunyonya kidole ni kuzuri au kubaya...piga kura hapo kulia.

2 comments:

Anonymous said...

kunyonya vidole ni mbaya kwa vile kuna watoto ambao hawaachi kunyonya kidole hadi wakubwa, ina haribu shape ya meno, mimi nilinyonya kidole hadi miaka 12 by the time nafikisha miaka 7 nilikua nina aibu sana lakini sikuweza kulala bila kunyonya kidole nilikua nagombezwa kwa vile nilikua nafanya shughuli na mkono mmoja ili kuulinda mkono ninaonyonya kidole, nilipata sana minyoo,kwa vile watoto wanacheza nje wanashika uchafu na wananyonya kidole,ndio maana kama mtoto ananza akiwa mdogo bora uumpe dummy!

Anonymous said...

Hii nimeipenda, wenyewe wamependeza. Mwanangu mimi anasumbua kunyonya hadi natamani kumfundisha kunyonya hicho kidole. Hata achoke vipi ni makelele kwakwenda mbele hadi usiku.