Wednesday, August 22

Siri za kumfanya mwanao awe na akili: Jifunze lugha!


Parlez-vous français? Do you speak English? Unazungumza Kiswahili? 
Kama umeelewa bofya kushoto hapo...


Wataalamu wanasema mtoto anayejifunza lugha zaidi ya moja huwa ana uwezo mkubwa wa kujielezea… au ndio maana wabongo tunajua sana kupiga siasa coz ya kiswanglish chetu?

Pia wanasema watoto wa aina hiyo huwa wanauwezo mkubwa wa kutatoa matatizo (problem solving), na kufikiri nje ya box, maana kwenye lugha mbalimbali wanakutana na tamaduni mbalimbali, hivyo kuwa na muono tofauti toauti kwenye vitu vingi.

Hata kama atajifunza hiyo lugha kwa muda mfupi tu utaona faida zake.

Ufanyeje?

Mwenzangu kufanya mwenyewe hili haiwezekani. Najua kama maneno 10 tu ya kifaranza, pamoja na kuisoma Form I na II, afu najua maneno matatu tu ya Kijerumani –lugha siziwezi tu!
Angalia utaratibu wa shule, hasa kama shule hizi za St. Academy basi mwanao atapata manufaa ya lugha ya kiingereza. 

No comments: