Wednesday, November 21

Jasmine 2nd Birthday Party

November 18 was a Lovely Sunday kwa mdau Jasmine kama anavyosema mwenyewe kwenye T-shirt yake! YES! alikuwa na kiparty uchwara cha kuadhimisha her second birthday! 


 hahaha, kweli it was a lovely Sunday, saaafi sana!

 Picha zinaweza kukuongopea ukadhani kulikuwa na party ya maana but ukweli ni kwamba aliwaalika swahiba zake wanne tu, Warda, Key, Rahma na Halima, wakaungana na her only brother, Jaffery, wakaivamia cake, wakaishambulia vilivyo, hadi tunakwenda mitamboni walikuwa bado wanapambana na cake!

Keki ikakatwa

pigeni makofi…… 

 hehehe, awejaaaa……(ndo nimewezaaaaa)

 J na J ni mtu na kakake hao (Jaffery na Jasmine) wakilishana tamtam
‘kula kaka’

Si akatia mgomo! Kisa? Kaka kakataa kuendelea kula!

Maskini kaka mtu alibembeleza mpaka kikaeleweka

Sasa anamlisha rafiki yake kipenzi Warda, mwenyewe anamwita da-wada

Kisha likafuata zoezi la kupiga picha, bofya hapo kushoto ujionee mapozi ya mdau, utachekajeeee? Usivunjike mbavu tu!

Tukutane 3rd Birthday Inshalah

No comments: