Friday, November 16

Migogoro ya wazazi inaathiri watoto



Wakati umeshakuwa na utashi, 

Je ulishawahi kushuhudia wazazi wako wanapigana au kufarakana? 
Ulijisikiaje? Nina imani hukujisikia vizuri kwani kiukweli inaumiza akili sana am sure.
Sasa basi wewe baba au mama mwenye familia na watoto kadhaa, mfanye nini pale kila mmoja limeshamkaba kooni la kwake na wadau wakiwepo? 


 Ni muhimu kuvumilia kidogo na kama inawezekana kuwaondoa wadau au nyie kutoka katika eneo waliopo kwani ni dhahiri kuwa migogoro ya wazazi kwa kiasi kikubwa sana inawaathiri watoto wetu. Kuna uwezekano wa watoto kuwa na emotional insecurity, huzuni wasiwasi na masuala fulani fulani katika maisha ya ujana. 

Kama uamini fanya utafiti utagundua kuwa: 
Watoto ambao wazazi wao wamekuwa wakigombana na kufarakana mara kwa mara tena mbele yao huwa  wana matatizo ya kihisia na akili. Unaweza kukuta tu mtoto hachangamani na wenzake au kama wanachangamana ni mkorofi na mgomvi kupita kiasi yani yeye haoni hatari mtoto kukatiza mbele yake akamfumulia mbali. Wengine kama wazazi wanapigana huku wanatukanana yale matusi yooooote aliyoyasikia huyaamishia kwa wenzake kama ni shuleni au mtaani wakati wanacheza.  
Kwahiyo basi kinachomata hapa sio kwamba nyinyi mnapigana na kufarakana. Bali ni namna gani mnafarakana na kupigana? 

Kama mnapigana kusemana vibaya na kufarakana hakikisheni kwamba mpo katika eneo ambalo mtoto hataweza kushuhudia kinachoendelea moja kwa moja. Kama mnajifungia chumbani dundaneni weeeeee mkitoka kila mmoja anapangusa uso halafu anaanza kumwita "Cleo mwanangu njooo" na kumwonyesha mapenzi yako yote kwani kiukweli ugomvi wenu haumuhusu. 

Ni muhimu kujifunza kuwa hapa watoto nafasi yao iko pale pale. haijalishi umedundwa una makovu umeumizwa au una kidonda rohoni mapenzi ya wadau yanapaswa kuwa pale pale kwani wazazi tulio wengi hushindwa ku control yanayotusibu na kuhamishia kwa mtoto. Atakula vinyungutu hadi ashike adabu yake, Kisa hasira za baba kakuudhi. Hii ni hatari sana na inawaharibu watoto kisaikolojia.
Mh hebu tushirikishane hapa, unapigana au kufarakana na na mwenzi wako? Umeshawahi kuwaza kama kupigana kwenu kunaweza kuathiri watoto?


No comments: