Friday, December 28

Ni Sahihi wadau kutuita majina yetu?

Ebu tujadili?
Unaonaje suala la wadau kutuita majina yetu?  
Ndio yetu, yale tuliyopewa na wazazi wetu.
Hii imekaaje kaaje?
Imekaa poa au vipi?
Zaidi zama kushoto

Nimeshuhudia watoto wengi wakishafikia adolescence huwaita wazazi wao kwa majina sio kwa ubaya la hasha bali kama Identification.

Yani Mfano:
Cleopatra : Christine (Mama), Cyprian(Baba) ameniambie nikwambie unipe pesa za kulipia tuition.
 au
Cleopatra: Akija Christine(Mama) nitamfikishia ujumbe.

Tujadiliane hapa zama kwenye comments.
 

4 comments:

Jiang said...

Nikiongezea tu hapo kwa Xtine: X wote wanawaita baba yao kwa jina...Xyleene anamwita 'tict', Xchyler alianza kwa kumuita 'chikch' ila sasa anamwita vizuri tu. Ba'mtu anaona poa tu. Kwa kweli na mie sioni ubaya wa hayo, naona iko poa ile mbaya, ingawa mie wanaligwaya jina langu, mana gumu halafu wala halikatiki! Loh!

Anonymous said...

Inategemea na culture unayowakuzia watoto wako.Kwa mfano kama kila kukicha baba anamwita mama kwa jina lake ni rahisi kwa watoto nao kufatisha!Kwa culture ya kitanzania kumuita baba/mama kwa majina yao si kawaida. Nakumbuka ilikuwa kumuita mama kwa jina lake unaweza kupigwa. But now things are changing au ni kwenda watoto wa kibongo kuwaita wazazi wao inakuwa kawaida.

Anonymous said...

Mimi kwaupande wangu naona poa tu kwani mtoto anajifunza kujua majina ya wazazi wake.

Nakumbuka kuna siku mtoto wa miaka mitatu alipotea ilichukua muda kujua alikotoka kutokana na mtoto yule kutojua majina ya wazazi. alijua baba na mama tu. Bahati nzuri alitokea mtoto anaeishi jirani yake ndo kumuokoa.

Mambo ya mila ngumu tuachane nazo tuchukue zile za muhimu tu.

Christine said...

Kwa kweli mimi natamani sana mwanangu akue ananiita jina langu ila dalili siioni kwa sababu hatuitani majina yetu, pia mtaaniwatu wengi wananiita Aunt hata saa nyingine Cleo ananogewa ananiita Aunt badala ya mama.