Monday, January 12

Ufahamu: Apple Linasaidia Mtoto Tumboni

Kula apple moja kila siku inaweza isiwe tatizo kubwa kwa wajawazito hata wale wasiojisikia kula, maana lina uchachu na utamu kwa pamoja, ila kitu ambacho wengi tusichojua ni faida zake kwa mtoto aliyeko tumboni.

Utafiti uliyofanywa karibuni unaonyesha kuwa mjamzito anayekula tunda la apple mara kwa mara wakati akiwa mjamzito anapunguza uwezekano wa mwanae kupata ugonjwa wa pumu, yes, ukila apple tu mwanao anaweza asipate pumu.

Watafiti waliofanya utafiti huo, uliofanyika Holland, wanasema bado hawajajua kwa nini apple linasaidia watoto wasipate pumu, ila wanahisi ni virutubisho vilivyopo ndani ya tunda hilo.
Usitake kujua inakuaje, we kazana kula maaaple tu!

1 comment:

shamim a.k.a Zeze said...

Ahsante mama X.... MH JINA LA MWANAO GUMU...MIE NAOMBA NIWE NALIKATISHA AU KAMA UNA A.K.A UNIAMBIE
...HII TIP YA APPLE IMENIKUNA NGOJA NIANZE LEO...KULA COZ SIKUMBUKI KAMA NIMEWAHI KULA HILI TUNDA TANDA NIMEJITWIKA HAKA KAMZIGO