Wednesday, August 12

Nimerudiii!

Hii ndio picha iliyokua inaniweka hai Berlin, nikifungua kompyuta tu naiona.
*****
Wadau nimerudi salama, jumamosi usiku...X alikua macho airport ananisubiri...alivyoniona nasubiri mizigo ndani wala hakusubiri nitoke, akakimbia mbio kunifata, aliingia hadi ndani!
Kwa kweli nilifurahi sana...
Nashkuru sana wadau wote kwa ushirikiano...sasa tegemeeni mambo makubwa zaidi.
Mama, nakushukuru sana kwa kunitunzia kipenzi changu, nimemkuta X ana furaha, ana afya, kazidisha utundu tu (nahisi anadhani yeye ni spiderman, maana anapanda kila sehemu, hadi madirishani), ambayo ni dalili ya mtoto mwenye afya njema, nisingeweza kufanya chochote bila wewe, your love is timeless, thank you for everything.

2 comments:

Anonymous said...

karibu saaaaana mama na mwana maana tulikuwa tumefulia kwa kukosa vionjo katika blog yetu hii.

shamim a.k.a Zeze said...

WELCOME BACK MAMA X