Thursday, September 10

Mtoto wa Mwaka Mmoja ana Mimba!

Mtoto Kang na tumbo lake lililombeba pacha wake.

Kang akiwa na wazazi wake.
*****
Madaktari nchini China walipigwa na butwaa pale walipogundua kuwa sababu ya ukuaji wa ajabu wa tumbo la mtoto wa mwaka mmoja aitwae Kang Mengru, ni kuwepo kwa mtoto ndani ya tumbo lake.
Madaktari waliamua kuvalia njuga tatizo la tumbo la mtoto huyo na kulifanyia vipimo vya CT na kukuta mtoto mwingine tumboni mwa kabinti hako.
Unajiuliza imekuaje...madaktari wanasema itakua ni pacha wa mtoto huyo ambaye alitunga ndani ya tumbo la mwenzake badala ya kuwa kwenye tumbo la mama yake.
Ila usiwe na wasiwasi, hali kama hii, ya pacha mmoja kukulia ndani ya pacha mwingine tumboni kwa mama yao huwa inatokea mara moja katika wanawake laki tano (500,000) wanaojifungua.
Na kuhusu mtoto Kang, madaktari wamesema watamfanyia upasuaji kuondoa mtoto huyo.

No comments: