Monday, February 2

Mtoto wa Kiume Atahiriwe Akiwa na Umri Gani?

Poll yetu ya kwanza kabisa ya mtoto wa kiume atahiriwe akiwa na umri gani imefungwa rasmi tarehe 31 january.
napenda kuwashkuru wale wote walioshiriki kupiga kura pale wanapoona ndio chaguo lao.
Hadi inafungwa poll hii ilipigiwa kura na watu 127.
Matokeo ya Mtoto wa Kiume Atahiriwe Akiwa na Umri Gani? ndio haya.
Kabla ya Arobaini: 41 (32%)
40 hadi Miezi Sita: 33 (25%)
Chini ya Miaka 2: 25 (19%)
Zaidi ya Miaka 2: 13 (10%)
Atajua Mwenyewa Akishakua: 15 (11%)

*****
Kutahiri kwa wanaume ni kuondoa kwa ngozi ya mbele ya uume. Utafiti wa mambo ya kale unaonyesha kuwa ilikua inafanywa tangu enzi za Misri ya Kale.

Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinakadiria kuwa asilimia 30 ya wanaume wote duniani wametahiriwa, ambapo kati yao, asilimia 68 ni waislam.

Kuna utata mkubwa hasa kwenye nchi zilizoendelea kuhusu kutahiriwa. Wanaounga mkono wanasema kuwa maumivu ya kutahiriwa ni kidogo ukilinganisha na na faida za kiafya zinazotokana na kitendo hicho.

Wakati wanaopinga suala hilo wanadai kuwa lina madhara kiafya hasa katika kujamiiana, na wanasema linakiuka haki za binaadam linapofanywa kwa mtoto ambaye hashiriki kwenye maamuzi hayo.

Utafiti na WHO wanakubaliana kwamba kutahiri mtoto wa kiume kunapunguza kwa kiwango kikubwa uwezekano wa wanaume waliotahiriwa kuambukizwa virusi vya ukimwi.
*****
Kwa kweli nimekosa utafiti unaoonyesha lini ni vizuri kutahiri mtoto ingawa watu wengi pamoja na madaktari wanasema ni vyema kumtahiri mtoto akiwa mdogo ili kupunguza maumivu as mtoto mdogo anakuwa bado hajui maumivu, au kitaalam wanasema senses zake zinakuwa mbali, bado hazijawa fully formed, ingawa huko nchi zilizoendelea wanasema kwamba maumivu hayana tofauti kati ya mtoto na mkubwa.

Nikiwa mama wa mtoto wa kiume, na mtu ambaye kwa kiasi kikubwa nategemea sana ushauri wa kitaalamu kufanya maamuzi yaliyosahihi, wataalam hawajanisaidia kabisa katika suala hili, hivyo basi ntatumia tamaduni zetu kufanya ninaloona ni sahihi.
*****
Narudia tena kuwashukuru wote mlioshiriki.

Poll mpya inakuja soon…

No comments: