Monday, November 2

Unatekeleza vizuri majukumu ya kazi yako ya ubaba?


Baaaaba, baaaaba, baaaba...

waaao!

Hii nimetumiwa na mdau Prisca Mbeswa anasema, "washua wa kibongo wakishakuwa viongozi wanasahau haki za kimsingi kabisaa za watoto wao,,,,

huyu angekuwa ni mtz ungeona jinsi ambavyo wangedhibitiwa na usalama wa taifa na ma bodyguard wadaku,,,,"

Mimi nakubaliana na Prisca kabisa, au madingi wa kibongo mnabisha???

Kwa kuanzia tu mi sijawahi kumuona JK akiwa karibu na familia yake kikawaida...kila kitu protocal, hata kwenye starehe wanaenda kiprotokali!

Kama baba jiulize, unatimiza wajibu wako katika kazi yako ya ubaba?

Mara ya mwisho umepokewa kama hivi na mwanao lini? ukute kila siku unaondoka wamelala, unarudi wamelala!

Mara ya mwisho umetoka na mwanao, ukatimia muda nae kuongea, kucheza, kucheka, kujuana lini? au we muda wako ni kukaa baa na washkaji tu? Miaka inaenda unadhani unamjua kumbe wala humjui mwanao, by the time unajua hilo unabaki kulalamika, hawa watoto wanamsikiliza mama yao tu!

Baba tenga muda wa kukaa na wanao, hata kama suti itachafuka kwa kuwa kakurukia na uchafu sawa tu, hamna kitu kizuri kama kuwa karibu na rafiki wa mwanao.

4 comments:

Mama Nadya said...

ha ha ha ha tena hapo mtoto angemrukia angemwambia hebu nenda kacheze kule na mama yako au na mdogo wako.....mie naenda jipumzisha...mwengine akiona bugza za watoto zimezidi ndipo wanapotafuta baa au nyumba ndogo wakapumzike...madai yake kule kuna fujo za watoto..

Bongo Pix said...

Uchonokozi huo bibie, afu hii ni kitu ambacho mtu anakuwa nacho toka zamani si cha kuiga.

Mababa wengine wakipata kanafasi kidogo familia ndo bye bye tena, hawamwoni, ukuiliza niko busy.

Anonymous said...

true true nimeipenda hii, wababa wakibongo mjifunze sio kupretend tu wageni wakija kujifanya wako close kumbe usanii mtupuu. Tena wanaume wakipata vyeo ndo kabisaaa watoto ni wa mama hata size za watoto hawajua au mtoto yuko darasa la ngapi none of his business damn busy dads muweke muda kwa watoto pia. ni aibu wala si ufahari.

Anonymous said...

Jamani mila zetu naona ni tofauti, huku toka mimba baba anafundishwa kuwa karibu na familia yake na usipokuwa karibu wanakusha ngaa coz kila mtu utamwona weekend na family wake hakuna mambo ya kuhang out sana bar na rafiki wako sababu huko tz wanaume wanapata company bar nakufanya nyumbani ni sehemu ya kulala ila furaha ni bar ndo sababu ya kukosa muda na hii inasababisha hata wale sio walevi waone aibu kuambatana na watoto cz haiko common utaoneka mkeo umetawaliwa nae.