Showing posts with label Baba na Mwana. Show all posts
Showing posts with label Baba na Mwana. Show all posts

Tuesday, December 4

Likizo Tym vipi?

Likizo imeshaanza...nyumbani lazima kuchangamke maana wadau wako home full time!
X ameianza kwa kasi sana...Ijumaa alitoka straight from class to Ubungo, alikua anaenda Morogoro kwa daddy...alisindikizwa na Anko, so it was boys only affair!

Likizo hii kuna wanaeonda kuhesabiwa...siku hizi si wachaga tu, kwenda kijijni wakati wa likizo raha sana, kuna wanaobaki hapahapa, kuna wanaenda abroad kutembelea ndugu na marafiki...whatever you are doing, hakikisha mdau ana-enjoy!
Likizo njema.

Friday, November 23

Baba wa Mfano

Mama na Mwana ilipishana na Baba wa mfano.

    Baba ana nafasi sana katika kumlea mtoto...si unaona mdau anavyofurahia hapo...
Kina baba mpo?


Monday, November 12

Xy's One year photoz

...hii ndio picha niliyompiga kwa ajili ya kumbukumbu ya kutimiza mwaka mmoja.

Vipi...ningeingiza kwenye shindano la photogenic Bebi ingeleta mchuano?




...hapa ndipo moyo wangu unapodunda! 

Tulipiga picha nyingi...Bofya hapo kushoto kuziona...Bahati mbaya mlengwa hakuwa kwenye mood...so hamna picha aliyocheka na pipi ndio ilikua inamfanya asilie!!!

Friday, August 10

Kama US president ana time, wewe unashindwaje?

...Yes, President Obama mwenyewe na mwanae mdogo, Sasha... Baba na Mwana moment.
...Rais wa nchi kubwa kama Marekani ana muda wa kukaaa kwenye majani kudekeza mtoto, afu wewe unajifanya uko bize... acha hizo, wikend ndio hiyo inanukia, tenga muda wa kukaa na mwanao wikend hii!

Tuesday, March 9

Fred &Michael

Mdau Fred Mukunza akiwa na baa yake Michael Mukunza.
so sweeeeeeeeeeeeeeeet!

Wednesday, December 16

Khloe- Dady's girl

Khloe akideka kwa baba'ke, Innocent Mfumu juzi juzi hapo alivyotimiza miezi mitatu kamili.
Wamependeza sana kiukweli...na huyu baba mtu anavyojidai na huyo mtoto, utadhani yeye ndio mtu wa kwanza kuwa na mtoto...maana hiyo miezi mitatu tumetangaziwa ofisini, na picha imepigwa (afu kaiphotoshop mwanyewe, nimeletewa), sipati picha besdei ya mwaka mmoja itakuwaje.
Hongera kwa kuwa baba, kumpenda mam'mtu (Rosemary Mallya) na kujidai na mwanao.

Friday, December 4

Amin akila good time na baba

Mdau Amin Riziky Danga (1.5yrs) wa Berlin, akifurahiii na baba yake Riziky Danga.

Hapa sijui wanaonyeshana nini, naona wako biiiize...sijui mdau anaelewa kiasi gani kwenye mambo anayofanya baba hapo...

Relaxing...!

Friday, November 13

Bridgitte, dady's girl

Mdau mpya, Bridgitte akiwa na bab'ke, kwa kweli hapo mama huna chako, unless wewe na baba muwe mmefanana!Na wamependeza sana!
Mam'tu Consolatha Ngowi ndio amegundua siri ya mtoto wa kike na baba anasema, "Jamani mtoto wangu huyu ni kipenzi cha baba,yaani kama anakula dad akiingia tu ujue ndo biashara itaishia hapo,atataka dad ndo amlishe! mara dad nibebe,unakuta hapo hata dad tai hajavua!!!nimegundua kuwa watoto wa kike na kipenzi cha baba."


Thursday, November 5

Andre & Ben

Andre Mwanambuu akiwa na baba yake Banjamin Mwanambuu, home kwao Kino.
Wamatoka bomba sana, maana baba anaonekana anamu-admire mwanae.

Monday, November 2

Unatekeleza vizuri majukumu ya kazi yako ya ubaba?


Baaaaba, baaaaba, baaaba...

waaao!

Hii nimetumiwa na mdau Prisca Mbeswa anasema, "washua wa kibongo wakishakuwa viongozi wanasahau haki za kimsingi kabisaa za watoto wao,,,,

huyu angekuwa ni mtz ungeona jinsi ambavyo wangedhibitiwa na usalama wa taifa na ma bodyguard wadaku,,,,"

Mimi nakubaliana na Prisca kabisa, au madingi wa kibongo mnabisha???

Kwa kuanzia tu mi sijawahi kumuona JK akiwa karibu na familia yake kikawaida...kila kitu protocal, hata kwenye starehe wanaenda kiprotokali!

Kama baba jiulize, unatimiza wajibu wako katika kazi yako ya ubaba?

Mara ya mwisho umepokewa kama hivi na mwanao lini? ukute kila siku unaondoka wamelala, unarudi wamelala!

Mara ya mwisho umetoka na mwanao, ukatimia muda nae kuongea, kucheza, kucheka, kujuana lini? au we muda wako ni kukaa baa na washkaji tu? Miaka inaenda unadhani unamjua kumbe wala humjui mwanao, by the time unajua hilo unabaki kulalamika, hawa watoto wanamsikiliza mama yao tu!

Baba tenga muda wa kukaa na wanao, hata kama suti itachafuka kwa kuwa kakurukia na uchafu sawa tu, hamna kitu kizuri kama kuwa karibu na rafiki wa mwanao.

Wednesday, October 28

Dady's girl: Ashlyn & Albinus

Mdau Ashlyn Kerya mikononi mwa baba Albinus Kerya.
Baba anabeba mtoto kwa uangalifu, dalili za huyo mtoto kuwa Dady's girl zinajionyesha mapema!

Friday, October 23

Ney & Micha

Mdau mpya Neema ameona na yeye ajidai na baba yake Micha.
Mtoto ni mzuri kwa kweli, cute, cute cute...na afya imekubali.

Tuesday, October 20

Proud Dady

Wadau Audery, Christian na Faraja wakiwa na baba yao.
Huyu mzungo katotoa knock out wabongo, maana kafanana nao wote watatu, katuachia rangi na nywele kwa mbaaaaali.

Friday, September 11

Arsenal Damu!

David & Noah Manata wa Denmark wanasema wao ni Arsenal damu.
Hapa na babab yao Frank Manata.

Wednesday, June 10

Wadau Mmependelea...

Baada ya kupitia comment zotee ka makini inaonyesha kuwa wadau wengi zaidi wanaona tuko 50/50, yani Xchyler amejitahidi kuwa mtoto mzuri na kuhakikisha ametuchanganya waote wawili, au kama kaka yangu Mwaipopo alivyosema, itakua akija kwetu wanasema amefanana na wajomba, akienda kwa baba wanasema amefanana na baba.
Lakini wengine wengi tu wamempendelea Sixtus na kusema yeye ndio ana damu kali zaidi, yani hamuwezi amini, wawili tu ndio wamesama ni mimi nna changu kidogo!
All in all, asanteni kwa kuamua ugomvi huo, na kwa sasa mshindi keshapatikana, ila round ya pili ni mwaka kesho, maana kuna wadau wa kutosha wamesema tusubiri hadi afikishe miaka miwili, na mpambano utapamba moto akizaliwa baby number last, Mungu akijaalia miaka miwili ijayo.

Sunday, May 24

Prosper & Deo- Proud Father

Deogratious Mushi akionekana ana furaha na mwane Prosper Mushi - cuuuute boy- ambaya alikuja kumcheck baba yake ofisini jana.

Thursday, May 21

Prince & Franco

Hapa lazima Prince alikua anadakwa asiende sehemu isiyotakiwa, maana mtoto akishaanza kutambaa ndio macho yote kwake saa zote, akiwa anakimbia kwa wale wanaopenda kupunguza mwili kumkimbiza nyimba nzima ni zoezi tosha.
Posted by Picasa

Sunday, May 17

Baba na Mwana Kariakoo



Posted by PicasaMsweeden aliyejitambulisha kama Hans Oisson akiwa amembeba binti yake Saba wakizungukia mitaa ya kariakoo hivi karibuni.
Swali: Wababa wa kibongo mnawezaaa? Kwanza kubeba mtoto mgongoni, pili kuzurura nae umbali mrefu toka home peke yako, mnaweza?
(Picha na Benard Rwebangira wa BongoPicha)

Wednesday, March 25

Baba na Mwana - Nasri & Charunga

Nasri akiwa na baba yake Charunga Ally, jamani mtoto kafanana na baba yake utadhani photocopy? mashavu, macho, pua mdomo, kila kitu!