Tuesday, March 13

Unataka kuwa kigori forever???

Wachina wana mambo....mie mwenzeni hii stori ndio nimeiona jana jioni...
Haya sasa wameleta mashine ya kusimamisha matiti (maziwa saa sita!) , kwa wale wasiopenda yaliyolala, yawe yalilala natural, kwa ajili ya kunyonyesha kina X, au basi tu uzee unakunyemelea.
Hapap hapa bongo unalipa hela si nyingi sana ni kuanzia laki na nusu (urembo gharama) unaanza kuvutwa, hadi kieleweke!
Habari iliyondikwa kwenye gazeti la Mwananchi la Jumapili inasema kuwa huduma hiyo ya kusimamisha matiti yaliyolala, imeanza kutolewa katika Saluni ya Blue Palace, iliyopo nyuma ya Shule ya Mapambano, Sinza jijini Dar es Salaam. (am sure hadi leo ishajaa watu)

Mashine yenyewe ndio hiyo...
Unaambiwa mashine hiyo inayoitwa ‘Beauty Machine’ ina uwezo wa kusimamisha matiti ya kila saizi kwa kuwa huambatanishwa na vibakuli (cups) kama unavyoona pichani hapo chini. Kazi kubwa ya mashine hiyo ni kuamsha misuli ambayo hushikilia nyama za matiti.

Mashine ya kusimamisha matiti kazini...


Haya kina mama na kina dada kazi ni kwenu!


2 comments:

Anonymous said...

Mie nauliza jamani baada ya hyo process hakuna madhara baadae?..maana mchina mmh!

Anonymous said...

ee makubwa! wapenda urembo saa 6 kazi kwenu, kizuri hakikoc kasoro baadae misuli ikilegea cndo yataanguka hadi miguuni,wakati mwingine ni bora m2 ubaki na ulichopekewa na Mwenyezi