Monday, December 10

Rotavirus yapata chanjo

Mama Salma Kikwete akitoa chanjo kwa mmoja wa watoto kuashiria uzinduzi wa chanjo mpya za “PVC 13 na Rotarix” kukinga watoto dhidi ya Nimonia na magonjwa ya kuhara.

Jamani, mnakumbuka mwaka huu mwezi April tulisumbuka sana na ugonjwa uitwao Rotavirus? Maana ulitikisa kwa kama wiki mbili, unasikia watoto mara wanne, mara sita wamakufa, ila kukawa hamna kinachoeleweka, hospitali wanasema hawaujui kama basi hofu tu. 
Kujikumbushia soma hizi MLIPUKO WA ROTAVIRUS na UPDATE yake.
Well, kama nilivyosema those daya kulikuwa hamna chanjo hapa nchini, now chanjo imekuja, soma hapo chinikuijua!


Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wiki imezindua chanjo mpya zinazolenga kukinga watoto dhidi ya nimonia na magonjwa ya kuhara yanayo sababishwa na kirusi cha Rotavirus.

Akizindua chanjo hiyo leo Mke wa rais Mama Salma Kikwete amesema kirusi cha Rotavirus kinachangia asilimia 18 ya vifo vya watoto vinavyotokana na kuharisha.

Amesema kuongezeka kwa chanjo hizi hapa nchini kutapunguza vifo vya watoto vitokanavyo na maradhi haya ili kufikia lengo la mileni namba 4 ifikapo 2015.

(Picha, story kwa hisani ya Dewji Blog)

1 comment:

Anonymous said...

afadhali inapatikana hospitali za wilayani kote nchini au vituo maalumu tu?