Showing posts with label Celeb Toto. Show all posts
Showing posts with label Celeb Toto. Show all posts

Friday, November 5

Kutana na Willow

Anaitwa Willow, ni product ya Will na Jada Smith...alianza kuonekana kwenye cover la kitabu cha ma'mtu...then tukamuona na style za ajabu za nywele hadi mavazi (nnachopenda ni nguo zinafaa kwa umri wake as zinamcover)...now ametoa wimbo wake mpyaaa, Whip my Hair umenikaa kichwani si mchezo...huyu ana kila dalili ya kuja kuwa super star!

 

...na hii ni style ya nywele inayonekana mwanzo tu wa wimbo wake...kama nayo naizimia vileeee, kwa kuiangalia tu, not wearing it.


 
Hii style ya suruali nimeipena flan...hadi za watu wazima zipo, so mafashstonista msiogope kujimwaga na wanenu, kwenye mini me kwa suruali hizi... wikend njema!


Friday, April 3

Shymaa na Gavana wa Australia

Shymaa akipokea zawadi toka kwa Gavana Mkuu wa Australia, Quentin Bryce alipokwenda kumuaga katika Hotel ya Kempinski. Shymaa ni mtoto wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dk. Batilda Burian (moja wa mawaziri wacheche nnaowazimia personally). (Picha na Lulu Mussa).

Saturday, January 3

Baba na Mwana - Thierry na Josh

Thierry Mukanda Murunga akiwa na baba yake Josh Murunga (mtangazaji wa EATV, pia producer wa vipindi vingi kwenye TV hiyo, including Planet Bongo). Kwa jina kama hili, hatuna shaka wewe ni ARSENAL damu, sijui nae huyu atakuwa striker? Mnaojua kugundua vipaji tangu mapema mnasemaje kuhusu hiyo miguu ye Thierry Murunga?

Monday, December 22

TZ First Children : Khalfan Kikwete

Mtoto Khalfan Kikwete akiongozana na baba yake Rais Jakaya Kikwete kutoka katika msikiti wa Al-Farouq Kinondoni baada ya kuhudhuria ibada ya Eid el Haj iliyofanyika kitaifa msikitini hapo.
(Ni kazi kidogo kupata picha za watoto wa kwanza wa bongo, ntakuwa nazipost kadri nnavyopata, as ni vizuri tuwafahamu na wao pia, sio tuwajue wa Bush na Obama tu. Hii kwa hisani ya Fadher Kidevu)

Saturday, December 20

Bongo Celeb Toto - Thierry Murunga

Thierry Mukanda Murunga mtoto wa mtangazaji maarufu wa EATV, Josh Murunga (pia producer wa vipindi vingi kwenye TV hiyo, including Planet Bongo) anatufungulia Celeb Toto ya hapa bongo. Mama yake ni Janeth Mushi. Huyu mtoto anaonekana mtundu kama baba yake, yani hapa ana miezi mitatu tu!

Monday, December 8

Binti wa Father Kidevu


Glory Mroki (miezi minne) mtoto wa blogger na mpigapicha maarufu, Mroki Mroki aka Father Kidevu anayepatikana http://www.mrokim.blogspot.com/. Jamani huyu mtoto m-cute!

Thursday, December 4

B'Day ya Mtoto wa Lil Wyne


Mtoto wa Lil Wyne, Reginae, leo alisherehekea Happy Birthday ya miaka sita. Baba yake alifanya bonge la pati, watu maarufu kibao walikuwepo, akiwemo T.I na wanae na Monica na mwanae.

Monday, December 1

U.S. First Family


Sasha (7yrs) na Malia (10yrs) wakiwa na baba yao, raisi mteule, Barrick na mama yao, The Next First Lady, Michelle, siku ilipotangazwa kuwa baba yao ameshinda kiti cha uraisi wa U.S. Kinachosubiriwa ni kuapishwa tu, sio mbali, ni next month tu.
Tetesi: Michelle anataka ajaribu tena, anatamani sana mtoto wa kiume.