Jumatatu hii, yaani jana, kwa mara ya kwanza nilienda kumuona Dr Massawe. Sina haja ya kuelezea kuhusu uzuri wa huyu doctor, kwa kweli nimeridhika na matibabu yake sana, sana, sana na wengi mnajua sifa zake, iwe kwa kuhadithiwa au kuexperience mwenyewe.
Tatizo langu ni ile kuwahi namba kunakotakiwa. Jumapili sisi hatukulala, tulikaa Coco Beach hadi saa sita usiku, ndo tukaenda (anyway, that was extreme, ila tulishaenda saa tisa usiku tukakosa namba, so tuliamua kuto-takechances). Mtu wa pili alifika kwenye saa nane na robo, na mtu wa mwisho alifika saa 10:05!!! Yes, wote waliofika baada ya hayo, ilikua imekula kwao, as walikua washachelewa namba.
Hii yote inatokana na nini? Demand, jamani. Maana mie kila nikiulizia naambiwa hamna kiboko kama Dr Massawe, na kwa kweli ni mzuri, ila
JE, MJI HUU, HAKUNA DAKTARI WA WATOTO MWINGINE MZURI KAMA DR MASSAWE?
Jamani tusaidiane, niandikie hapa kwenye comment dokta gani mwingine unayemfahamu ambaye ni mzuri kama Massawe, tupe jina, anakopatikana, na exerience yako...ni vistory vya kumpeleka mtoto kila hospitali akashindikana, afu Massawe akakuta ni allergy tu vinavymfanya Massawe awe juu.
Kama story yako ni ndefu sana unaweza kutuma kwanye mamanamwana@gmail.com
Then, nitaweka post nyingine ya kushare kina Massawe wengine wa mji huu, mlionifriend Facebook, huu mjadala ulikua mrefu sana huko, kwa faida ya wengi nimeuhamishia huku!
Naomba ieleweke kwamba nia ya hii post sio kumpunguzia Massawe wateja, am sure anamore than he needs, ila ni kutupa wazazi options ya kutolazimika kukesha (pia am sure hapendi tukeshe ndio maana kuna tangazo la kutokesha pale mlangoni kwake) kwa kujua madaktari wengine wa watoto wazuri ambao wanaweza kuwatibu wanetu tukaridhika.